Atabatu Abbasiyya tukufu imetengeneza barakoa zaidi ya laki nne (400,000) na imezigawa bure

Maoni katika picha
Idara ya ushonaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa kitengo cha usonaji wa barakoa kimefanikiwa kushona zaidi ya barakoa laki nne (400,000) baada ya kuongeza uzalishaji kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Korona katika mkoa wa Karbala na Iraq kwa ujumla, watumishi wa kitengo hicho wanafanya kazi kwa bidii kubwa, husunan baada ya barakoa kuadimika kwenye vituo vya afya, barakoa zote wamegawa bure kwa watu mbalimbali, wakiwemo watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), askari na wahudumu wa afya na wengineo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya ushojani Ustadh Abduzuhura Daud Salmaan, amesema kuwa: “Mafundi wa kitengo cha ushonaji wamepata uzowefu mkubwa wa kushona barakoa ambazo zinahitajiwa na kila mtu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, uzowefu wao unaongezeka siku baada ya siku na unaonekana wazi kwa kuongezeka idadi ya uzalishaji wa Barakoa kila siku, walianza kazi ya ushonaji wa barakoa hizo tangu siku ya kwanza ulipo tangazwa umuhimu wake”.

Akaongeza kuwa: “Wanaendelea na kazi bila kupumzika, Atabatu Abbasiyya imetupa kila tunacho hitaji katika ushonaji wa barakoa, pamoja na kuadimika vitambaa vinavyo faa kushonea barakoa lakini Ataba imehakikisha sisi hatukosi vitambaa hivyo, tunatumia vitambaa bora vilivyo thibitishwa na idara ya afya, havizuwii wala kusumbua wakati wa kupumua, tunashona ukubwa tofauti zinazofaa kwa watu wa kila umri”.

Akasisitiza kuwa: “Tunaendelea na kazi bila kuchoka, tunajitahidi kushona idadi kubwa kadri tuwezavyo, mafundi wetu wanafanya kazi kama nyuki, kila mmoja na jukumu lake, kama hali ikiendelea kuwa kama ilivyo sasa tunatarajia kuongeza uzalishaji siku za mbele –Insha-Allah-”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imechukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafanyia kazi maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya, na ushonaji wa barakoa ni moja ya kufanyia kazi maelekezo hayo na kusaidia kutoadimika bidhaa hiyo sokoni kutokana na wingi wa uhitaji wake kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: