Upimaji wa vifaa vya ujenzi umekuwa na matokeo muhimu kwenye miradi ya majengo

Maoni katika picha
Upimaji wa vifaa vya ujenzi ni moja ya sekta muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye miradi ya majengo, wana vifaa vya kisasa vinavyo wawezesha kutekeleza jukumu lao kwa ufanisi, hadi baadhi ya vituo vya serikali na binafsi huja kwetu kupima vifaa vyao vya ujenzi, kwa sasa kituo chetu ni miongoni mwa vituo bora katika sekta hiyo.

Mkuu wa kituo cha upimaji wa vifaa vya ujenzi chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi, Mhandisi Ammaar Adnani amesema kuwa: “Kituo chetu kinapima, tofali, nguzo, marumaru, nondo na kila kitu kinacho tumika kwenye ujenzi”.

Akasema: “Watumishi wa idara hiyo wana uzowefu mkubwa, pia wamehudhuria warsha na mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo, ili kuwapa ujuzi zaidi wa kutumia vifaa vya kisasa walivyo navyo”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kila iwezalo ili iweze kufikia hatua ya kujitegemea katika kila sekta, hususan sekta ya miradi ya kihandisi ambayo ni kiungo muhimu katika kuwatumikia wananchi wa Karbala na miradi ya Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: