Ofisi ya Marjaa Dini mkuu imetoa wito kwa wananchi wa Iraq kuongeza tahadhari na ulazima wa kuendelea kujikinga

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu imetoa wito kwa wananchi wa Iraq kuongeza tahadhari na ulazima wa kuendelea kujikinga na maambukizi.

Hayo yapo katika tamko la siku ya Jumamosi asubuhi (13 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (6 Juni 2020m), ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Enyi wairaq watukufu

Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu na baraka zake

Katika siku hizi ngumu ambazo inaendelea kuongezeka idadi ya maambukizi ya virusi vya (Korona) katika miji tofauti kwa namna isiyokuwa ya kawaida –hususan katika mji mkuu wa Bagdad- kwa mara nyingine tena tunakuombeni muongeze tahadhari, tunasisitiza ulazima wa kujikinga na maambukizi kama ilivyo elekezwa na sekta zinazo husika, kama vile kujiepusha kushikana na watu, kukaa kwa umbali uliotajwa na idara za afya, kuvaa barakoa na kunawa mikono au kuvaa soksi za mikonano na mengineyo.

Hakika kuzingatia maelekezo hayo na mengine kama yalivyo tolewa na wataalamu wa afya, kunasidia kupunguza maambukizi ya virusi, hivyo haifai kupuuza na kudharau maelekezo hayo, ukizingatia taifa limeelemewa na wingi wa watu walio ambukizwa, ambao wamejaa katika hospitali nyingi.

Hakika mapambano ya janga hili ni jukumu la kila raia na kiongozi, kila mmoja anatakiwa atekeleze wajibu wake, na washirikiane kuvuka kipindi hiki kigumu kwa hasara ndogo.

Tunawakumbusha kuwa madaktari na wauguzi wanafanya kazi kubwa ya kuwatibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona, wao na familia zao wapo katika hali ngumu sana, hakuna wajuao hilo ispokua wachache, bali uhai wao upo hatarini kutokana na kazi zao, idadi ya maambukizi kwa wauguzi na madaktari imeongezeka hivi karibuni, lazima kila mtu awaonee huruma kwa kuongeza umakini wa kujikinga na maambukizi, ili kupunguza idadi ya maambukizi mapya na kuwapa nafuu katika utendaji wa kazi zao.

Hakika tunawapongeza sana na tunabusu mikono yao kwa kazi kubwa wanayo fanya ya kuhudumia wananchi na kutekeleza wajubu wao kitaifa na kibinaadamu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awalinde na awape kila la kheri, afya na baraka, pia tunamuomba Allah mtukufu awaponye haraka wagonjwa na aondoe janga hili hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: