Ofisi ya Marjaa Dini mkuu: lazima tuheshimu na kufuata malekezo ya kujinga na maambukizi yanayo tolewa na sekta husika

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, imehimiza ulazima wa kuheshimu na kufuata maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona yanayo tolewa na sekta husika.

Hayo yapo katika tamko alilotoa asubuhi ya Jumamosi (13 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (6 Juni 2020m), lifuatalo ni tamko kuhusu jambo hilo:

Katika siku hizi ngumu ambazo inaendelea kuongezeka idadi ya maambukizi ya virusi vya (Korona) katika miji tofauti kwa namna isiyokuwa ya kawaida –hususan katika mji mkuu wa Bagdad- kwa mara nyingine tena tunakuombeni muongeze tahadhari, tunasisitiza ulazima wa kujikinga na maambukizi kama ilivyo elekezwa na sekta zinazo husika, kama vile kujiepusha kushikana na watu, kukaa kwa umbali uliotajwa na idara za afya, kuvaa barakoa na kunawa mikono au kuvaa soksi za mikonano na mengineyo.

Hakika kuzingatia maelekezo hayo na mengine kama yalivyo tolewa na wataalamu wa afya, kunasidia kupunguza maambukizi ya virusi, hivyo haifai kupuuza na kudharau maelekezo hayo, ukizingatia taifa limeelemewa na wingi wa watu walio ambukizwa, ambao wamejaa katika hospitali nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: