Marjaa Dini mkuu amesisitiza ulazima wa kuwapunguzia kazi wahudumu wa afya kwa kuongeza umakini wa kufuata malekezo ya kujilinda na maambukizi ili kupunguza idadi ya maambukizi mapya.
Hayo yapo kwenye tamko alilotoa siku ya Jumamosi asubuhi mwezi (13 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (6 Juni 2020m), lifuatalo ni tamko kuhusu jambo hilo:
Tunawakumbusha kuwa madaktari na wauguzi wanafanya kazi kubwa ya kuwatibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona, wao na familia zao wapo katika hali ngumu sana, hakuna wajuao hilo ispokua wachache, bali uhai wao upo hatarini kutokana na kazi zao, idadi ya maambukizi kwa wauguzi na madaktari imeongezeka hivi karibuni, lazima kila mtu awaonee huruma kwa kuongeza umakini wa kujikinga na maambukizi, ili kupunguza idadi ya maambukizi mapya na kuwapa nafuu katika utendaji wa kazi zao.
Hakika tunawapongeza sana na tunabusu mikono yao kwa kazi kubwa wanayo fanya ya kuhudumia wananchi na kutekeleza wajubu wao kitaifa na kibinaadamu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awalinde na awape kila la kheri, afya na baraka, pia tunamuomba Allah mtukufu awaponye haraka wagonjwa na aondoe janga hili hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.