Nadwa kwa njia ya mtandao kuhusu nafasi ya malikale na wito wa kushiriki kwenye nadwa hiyo

Maoni katika picha
Nadwa zinazo fanywa na vituo ambavyo viko chini ya maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kwa njia ya mtandao zinaendelea, kituo cha upigaji picha wa nakalakale na faharasi chini ya maktaba kimekusudia kufanya nadwa ya kitaalamu chini ya anuani isemayo (nafasi za malikale katika tafiti za kielimu), kwa kushirikiana na mkuu wa kitivo cha malezi na taaluma za kibinaadamu katika chuo kikuu cha Karbala.

Mkuu wa kituo Sayyid Swalahu Siraji ameongea kuhusu nadwa hii akasema kuwa: “Hakika hii ni nadwa muhimu iliyo pangwa kufaywa na kituo chetu tangu zamani, lakini kutokana na mazingira ya sasa ya uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona, tumelazimika kutumia jukwaa la mitandao ya mawasiliano ya kijamii ili kuendeleza harakati zetu, nadwa inazungumzia utambuzi wa malikale na mambo muhimu katika tafiti za kielimu, kwani malikale ni moja ya misingi muhimu ya taarifa za kihistoria”.

Akaongeza kuwa: “Wahadhiri wa nadwa hiyo ni (Dokra Murtadhwa Nasrullah makamo mkuu wa mambo ya kielimu katika kitivo, Ustadh Ahmad Muhammad Abudi kiongozi wa kitengo cha faharasi katika kituo na Ustadh Muhammad Baaqir Muwafiq Zubaidi kiongozi wa kitengo cha malikale katika kituo, kutakua na shuhuda za washiriki ambazo zitatumwa kwa barua pepe”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunatoa wito kwa walimu na watafiti wajitokeze kushiriki kwenye nadwa hii itakayo fanywa Jumanne ya tarehe (9/6/2020) saa tisa jioni kupitia jukwaa la program ya (GOOGLE MEET) kila anayependa kushiriki ajiunge kupitia link ya nadwa ifuatayo: https://meet.google.com/iihodtyruh
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: