Mwezi kumi na tano Shawwal ni kumbukumbu ya kifo cha simba wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Maoni katika picha
Siku ya mwezi kumi na tano Shawwal inasadifu kifo cha Hamza bun Abdulmutwalib (a.s) Ammi wa Mtume (s.a.w.w), Mtume alihuzunika sana kwa kifo chake kilicho tokea mwaka wa tatu hijiriyya katika vita ya Uhudi.

Naye ni miongoni mwa maswahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na alikua miongoni mwa baba (Ammi) zake wema, kwa kauli ya Mtume (s.a.w.w) pale alipo sema: (Mbora katika ndugu zangu ni Ali, na mbora katika baba (Ammi) zangu ni Hamza –r.a-).

Sayyid Muhammad Amiin katika kitabu chake cha (Aáyani Shia) katika kumuelezea Hamza bun Abdulmutwalib anasema: “Aliuwawa siku ya Jumapili, aliye muuwa na Wahshiyyu bun Harbi, alikuwa ni mtumwa wa kihabeshi mwenye shabaha sana ya kurusha mikuki, waarabu walikuwa sio wataalam wa mikuki, bali yeye alikuwa bingwa wa kurusha mikuki”.

Katika kitabu cha tafsiri Qummiy imeandikwa kuwa: (Wahshi alikuwa ni mtumwa wa Jubair bun Mutímu Habashiyya, Wahshi alisema Muhammad simuwezi na Ali ni mtu mwenye tahadhari sana anageukageuka, nikamuangalia Hamza nikamuona anaelekeza watu, nikashika vizuri mkuki wangu nikamrushia ukamchoma akaanguka chini na kufariki, nikamfuata na kupasua tumbo na kutoa ini lake halafu nikampa Hindu, nikamuambia hili hapa ini la Hamza, akachukua na kuweka mdomoni kwake, Mwenyezi Mungu akalifanya kuwa kama jiwe akalitema na kulitupa, Mwenyezi Mungu akawatuma malaika wakalichukua na kulirudisha sehemu yake, Abu Abdillahi (a.s) anasema Mwenyezi Mungu hakutaka sehemu ya mwili wa Hamza iingie motoni, Hindu akamfuata Hamza na akakata masikio yake akatengeneza mkufu na akauvaa shungoni kisha akamkata mikono na miguu).

Baada ya kuisha vita, Mtume (s.a.w.w) akasema: (Mtafuteni Hamza). Akatoka swahaba kwenda kumtafuta, akamkuta Hamza akiwa kakatwa viungo vyake na kalala vumbini, kisha akamtuma swahaba mwingine na mwingine, kila aliyetumwa alimkuta Hamza akiwa katika hali ileile, na hawakurudi kumuambia Mtume (s.a.w.w), alipo ona wamechelewa kurudi akasema: (Naenda kumtafuta mwenyewe). Alipomuona akiwa kalala mchangani kwa tumbo huku muili wake umekatwakatwa, Mtume (s.a.w.w) alilia halafu akasema: (Sitapata mfano wako milele, sijafikwa na jambo zito kama hili).

Kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) anasema: (Mtume (s.a.w.w) alimzika Ammi yake Hamza kwa kutumia nguo zake akiwa na damu zake, akamfunika kwa shuka yake, likawa fupi miguuni akamfunika kwa majani, akamswalia swala sabini na akamsomea takbira sabini).

Kutokana na tukio hilo Ustadh Ali Swafaar Karbalai ameandika kaswida kuhusu kifo chake iitwayo (Tudul-Ibaa):

Ewe Hamza wa utukufu wa tuudal-Iba

Ewe bendera umewekwa juu kwa utukufu (nuswiba)

Ewe mwenye meno makali unapouma

Ewe mpiganaji hodari unapo pigana
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: