Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu inaiwezesha link yake kufanya kazi kwenye toghuti ya maktaba ya chuo kikuu cha Mosul

Maoni katika picha
Kituo cha taaluma za namba chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekubaliana na chuo kikuu cha Mosul kuwezesha link yake kutoa huduma za bure kwenye mtandao rasmi wa chuo kikuu cha Mosul, chini ya ushirikiano wa kielimu na kimaarifa kati ya pande mbili na umuhimu wa maarifa kwa wote.

Tumeongea na mkuu wa kituo cha taaluma na namba Ustadh Hussein Jawadi amesema: “Baada ya kuweka huduma ya kuazima vitabu kwa njia ya mtandao na huduma ya kutambua kiwango cha matumizi, huduma ambazo zimekuwa na matokeo mazuri kwa wakufunzi na wanafunzi wa vyuo, inaunganisha makumi ya wanafunzi kila siku na kuimarisha uhusiano kwa kuiwezesha link yetu kutoa huduma kwenye toghuti yao, ili kuwanufaisha wanafunzi wa vyuo vya Iraq”.

Jawadi akaongeza kuwa: “Kituo chetu kipo tayali kutoa huduma kwa kila anayependa kusaidia safari ya elimu na utamaduni hapa nchini na kulinda malikale za Iraq, ndio maana tumeweka makubaliano maalum na chuo kikuu cha Mosul ili kuwaunganisha na miradi yetu ya kitaifa, inayo husu kuhifadhi turathi zetu zilizo telekezwa na kushambuliwa na magaidi wa Daesh”.

Kumbuka kuwa Maktabatu Abbasiyya imekuwa kituo muhimu cha watafiti na wanafunzi, wanamiminika hapo kwa ajili ya kujisomea mambo tofauti, dini, historia, sayansi, malikale na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: