Waziri wa mafuta ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na katibu mkuu

Maoni katika picha
Waziri wa mafuta wa Iraq Ustadh Ihsani Abdujabaar Ismaili akifuatana na ujumbe wake baada ya Adhuhuri ya siku ya Jumatatu mwezi (15 Shawwal 1441h) sawa na (8 Juni 2020m), ametembelea malalo ya Abulfadhim Abbasi (a.s), baada ya kumaliza ibada ya ziara na dua amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar, pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo.

Wakajadiliana mambo mengi miongoni mwa mambo hayo ni kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa hii ni ziara ya kwanza kufanywa na waziri wa mafuta katika mkoa wa Karbala tangu apate madaraka hayo, aidha ametembelea pia mtambo wa kusafisha mafuta uliopo mkoani hapa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: