Maktaba ya wanawake inasaidia sekta ya elimu na tafiti kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa maktaba ambazo zimeendelea kutoa huduma katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na changamoto za maradhi hayo, milango yake imebaki wazi kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi na watafiti, ukiwa kama mchango wake katika kusaidia sekta ya elimu na utafiti pamoja na kuandaa warsha na nadwa mbalimbali.

Mtandao wa Alkafeel umeambiwa maneno hayo na kiongozi wa maktaba ya wanawake bibi Asmaa Abadi: “Maktaba imeandaa ratiba maalum inayo endana na mazingira yaliyopo, ambapo inatumia mitandao ya mawasiliano ya jamii na kutoa huduma masafa, ili kuendelea kuwasiliana na wakufunzi na wanafunzi pamoja na ugumu wa mazingira yaliyopo kwa sasa, tumefungua mitandao maalum kwa ajili ya jambo hilo”.

Akaendelea kusema: “Harakati hizi zinatokana na umuhimu wa kusaidia watafiti na kuweka mazingira mazuri ya kujisomea sambamba na kushawishi kila mwanafunzi akamilishe masomo na tafiti zake”.

Akabainisha kuwa: Huduma zinazo tolewa na maktaba ya wanawake kwa wanafunzi na watafiti wa kike kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii, zinalenga kuboresha sekta ya malezi na kupambana na mazingira yaliyopo, pamoja na kuonyesha umuhimu wa sekta ya elimu, mambo haya yanafanywa chini ya anuani isemayo (warsha za kielimu) kwa kupitia mawasiliano yafuatayo:

  • - Jukwa la mawasiliano ya mitandao ya kijamii.
  • - Barua pepe ya: net/ -library – women-.
  • - Kitengo cha maktaba: https://forums.alkafeel.net/node/884278
  • - Ukurasa wa maktaba ya wanawake kwenye facebook: https://www.facebook.com/lib.alkafeel

Kumbuka kuwa idara ya maktaba ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya inaenda sambamba na maendeleo ya dunia katika sekta hiyo, inajulikana kwa kufanya miradi ya kujenga uwelewa na uzalendo wa Dini na daifa pamoja na kulinda utamaduni, aidha inajitahidi kuimarisha uhusiano baina yake na vyuo vikuu pamoja na taasisi za Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: