Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi ametangaza kuwa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kwenye kituo cha Zaharaa (a.s) cha magonjwa ya tumbo kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu mkoani Karbala.
Akaongeza kuwa: “Kituo hiki kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1000), kinajengwa kwa kufuata ramani iliyopendekezwa na wanufaika na inayokidhi vigezo vya afya, pamoja na kuzingatia masharti yote ya afya wakati wa utekelezaji wa mradi”.
Akasisitiza kuwa: “Hakika mradi huu utakamilika ndani ya muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma, pamoja na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kutokana na kuongezeka idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona”.
Kumbuka kuwa kutokana na maelekezo ya moja kwa moja ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na muongozo wa Marjaa Dini mkuu wa kutaka isaidiwe sekta ya afya, Atabatu Abbasiyya tukufu ilijenga vituo vitatu vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.
Vituo hivyo ni:
Kwanza: kituo cha Alhayaat cha kwanza katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, kimejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1550), kinavyumba vya wagonjwa (56) pamoja na vyumba vingine vinne vya ofisi, dawa na usafi, kituo hicho kilijengwa na kukamilika ndani ya muda wa siku (15) tu.
Pili: kituo cha Alhayaat cha pili ambacho kilijengwa katika hospitali kuu ya Hindiyya kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (2m1500) kina vyumba (35) pamoja na vyumba vingine vya usafi na dawa, kilijengwa na kukamilika ndani ya muda wa siku (24) tu.
Tatu: kituo cha Alhayaat cha tatu kilicho jengwa na hospitali ya Amirulmu-uminina (a.s) katika mkoa wa Najafu kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo chake cha usimamizi wa kihandisi, kilikamilika ndani ya muda wa siku kumi na nane tu, kinaukubwa wa mita za mraba (600), kinavyumba (24) vyenye huduma zote muhimu pamoja na vifaa tiba.