Kituo cha habari na masoko Alkafeel kimempokea waziri wa vijana na michezo na kujadili kuhusu kuboresha uhusiano baina yao

Maoni katika picha
Kituo cha habari na masoko Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Jumatano (10 Juni 2020m) kimetembelewa na waziri wa vijana na michezo Sayyid Adnani darjani na ugeni alio fuatana nao, ambao ni mkurugenzi pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala na makamo wake, ujumbe huo kutoka wizarani umepokewa na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tumeongea na mkuu wa idara hiyo Ustadh Muhammad Aali Taajir amesema kuwa: “Ziara hii ya waziri wa vijana na michezo imetupa fursa ya kujadili mambo yanayo kiunganisha kituo chetu na wizara ya vijana, ikiwa ni pamoja na sekta ya michezo hapa Iraq, na kushirikiana na chama cha mpira wa miguu”.

Akaongeza kuwa: “Tumekubaliana kuimarisha ushirikiano na wizara katika sekta ya matangazo au matamko ya kwenye mitandao chini ya sheria za michezo kimataifa”.

Akaendelea kusema: “Aidha wamejadili kuhusu utambulisho wa sheria za taasisi za michezo ambazo zipo chini ya wizara ya vijana na michezo, ili kunufaika na uzowefu wa kituo katika sekta hiyo, ukizingatia kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ndio ya kwanza kuunda taasisi rasmi ya michezo hapa Iraq”.

Akasema: “Mheshimiwa waziri na wageni aliofuatana nao ametembelea kitengo cha uzalishaji wa vipindi pamoja na vitengo vingine, akasifu huduma zinazo tolewa na kituo hicho”.

Akamaliza ziara yake kwa kukabidhi cheti maalum cha Ataba tukufu kwa waziri wa na ugeni alio fuatana nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: