Atabatu Abbasiyya tukufu inaanza ujenzi wa kituo cha tano cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona jijini Bagdad

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema kuwa kitengo cha usimamizi wa miradi ya kihandisi kimeanza kujenda kituo cha tano cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.

Akaongeza kuwa: “Kituo hicho kinajengwa katika hospitali ya Ibun Qafi kwenye mtaa wa Alghadiir/ katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (5000)”.

Tambua kuwa miradi hii inatokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi pamoja na muongozo wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: