Hospitali ya rufaa Alkafeel na wizara ya vijana na michezo wamesaini makubaliano ya kuwatibu wanamichezo

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imesaini makubaliano na wizara ya vijana na michezo ya kuwatibu wanamichezo na viongozi wa wizara.

Wamekubaliana kutengeneza vitambulisho vya wafanyakazi wa wizara ya vijana na michezo.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara aliyo fanya waziri wa vijana na michezo Sayyid Adnani Darjali pamoja na ujumbe alio fuatana nao, akiwemo katibu mkuu wa wizara pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala na makamo wake leo siku ya Jumatano (10 Juni 2020m).

Makubaliano hayo yametangazwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ndani ya hospitali hiyo.

Fahamu kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekuwa ikitowa matibabu bora kwa vifaa tiba vya kisasa daima, kutokana na kuwa na vifaa tiba hivyo pamoja na madaktari bingwa wa kitaifa na kimataifa, jambo ambalo limeifanya itowe ushindani mkubwa kwa hospitali zingine za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina zote waliopo katika hali zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: