Waziri wa vijana na michezo ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na katibu mkuu

Maoni katika picha
Waziri wa vijana na michezo Ustadh Adnani Darjali siku ya Jumatano ya mwezi (17 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (10 Juni 2020m) akiwa pamoja na ujumbe alio fuatana nao, amefanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumaliza kufanya ziara na kusoma dua alikutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amesema kuwa: “Tumepata nafasi ya kujadili mambo mengi katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, akaeleza pia mtazamo wa Atabatu Abbasiyya tukufu kuhusu tabaka la vijana pamoja na harakati zinazo lenga tabaka hilo muhimu hapa nchini, aidha akaonyesha uwezekano wa kuwepo ushirikiano baina ya wizara na Ataba katika harakati zinazohusu vijana”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo katika mji wa Karbala, asubuhi ya leo siku ya Jumatano mwezi (17 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (10 Juni 2020m) imesaini makubaliano ya ushirikiano kati yake na wizara ya vijana na michezo ya kuwatibu wanamichezo na viongozi wa wizara ya vijana na michezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: