Hatua ya kwanza ya kazi ya ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha nne zinaendelea katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea na kazi za awali katika ujenzi wa kituo cha nne mkoani Karbala, kinacho jengwa kwenye kituo cha Zaharaa (a.s) cha maradhi ya tumbo katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi mtendaji wa mradi Muhammad Mustwafa Twawiil, akasema: “Hatua ya kwanza ya mradi inahususha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (1000), inakazi zifuatazo:

  • - Kusawazisha eneo la mradi.
  • - Kuondoa udongo wa juu kwa kina cha (sm 50) katika sehemu ya mradi.
  • - Kujenga tabaka la msingi kwa kutumia mawe makubwa.
  • - Kujenga tabaka la msingi kwa kutumia zege”.

Akafafanua kuwa: “Vifaa vyote vinavyotumika kwenye ujenzi vimekidhi vigezo vya kihandisi, vimetoka kituo cha Al-Atwaa ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya kwa ujazo wa mita za mraba (500)”.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya pili itahusisha kuandaa sehemu hiyo kwa kujenga msingi na kumwaga zege”.

Akasisitiza kuwa: “Eneo la mradi kwa mujibu wa ratiba ya wanufaika litakuwa na sehemu mbili, sehemu ya kwanza itakuwa ya maabara na ya pili itakuwa ya kutoa matibabu kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona”.

Kumbuka kuwa kituo cha Alhayaat cha nne ni sehemu ya vituo vitatu vilivyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vituo kama hivyo vitajengwa katika mkoa wa Bagdad na Samawa, pia ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya kukamilisha vituo vilivyo tangulia, kimoja kilijengwa katika mji wa Imamu Hussein wa kitabibu na kingine katika hospitali kuu ya Hindiyya mkoani Karbala, na kituo cha tatu kilijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: