Kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (140) kutoka mikoa (14): Tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu limefungua mafunzo ya Quráni kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (140) wenye umri tofauti kutoka mikoa (14) ya Iraq, Maahadi ya Quráni tukufu kupitia tawi lake la Najafu imefungua masomo ya hukumu za tajwidi na usomaji sahihi wa Quráni.

Haya yamesemwa na mkuu wa tawi hilo Sayyid Muhandi Majidi Almayali, akaongeza kuwa: “Tawi letu limezowea kufanya semina za Quráni katika mambo tofauti, ndani ya kipindi cha mwaka mzima, lakini kutokana na mazingira ya sasa pamoja na kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya sambamba na muongozo wa Marjaa Dini mkuu wa kujiepusha na misongamano, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tumeamua kufanya semina kwa kutumia intanet, ikiwemo semina hii chini ya ukufunzi wa Ustadh Ahmadi Zamili itakayo fanyika siku nne kwa wiki, watafundishwa hukumu za tajwidi na usomaji sahihi”.

Akaongeza kuwa: “Usomaji sahihi watafundishwa kila siku ya Ijumaa na Jumapili, na hukumu za tajwidi kila siku ya Jumamosi na Jumanne saa kumi Alasiri, watafundishwa hukumu za usomaji sahihi wa Quráni kuanzia matamshi ya herufi sifa zake na hukumu zake”.

Akafafanua kuwa: “Namna ya kushiriki katika mafunzo haya ni kwa kutumia mitandao yetu ya intanet au mtandao wa Alkafeel, kwa kutumia njia maalum itakayo chaguliwa na mshiriki ambayo ataweza kupokea masomo kwa urahisi, tumesha pokea maombi mengi, tutayafanyia kazi siku zijazo kwa kufungua semina zingine za masomo haya haya au mengine”.

Akamaliza kwa kusema: “Hii ni moja ya semina nyingi zinazo fanywa na tawi la Maahadi, kwa lengo la kuongeza uwezo wa usomaji wa Quráni kwa kufuata hukumu za usomaji wa tajwidi”.

Kumbuka kuwa semina zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni rukufu ni miongoni mwa harakati za Maahadi hiyo na zinapewa umuhimu mkubwa kutokana na faida yake, ya kutengeneza kizazi cha watu wanaosoma Quráni rukufu kwa ufasaha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: