Kumbukumbu ya sita kuhusu ushindi wa Iraq.. fatwa na mwitikio wa raia wa Iraq

Maoni katika picha
Siku kama ya leo tarehe kumi na tatu Juni 2014.. miaka sita iliyopita, ndani ya haram takatifu ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwenye mimbari ya swala ya Ijumaa ulitolewa wito wa Marjaa Dini mkuu wa kuiokoa Iraq na ulimwengu kutokana na hatari ya magaidi wa Daesh..

Wito wa Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Hussein Sistani ulisema kuilinda Iraq na maeneo matakatifu dhidi ya magaidi wa Daesh kuwa ni wajibu kifaya, sambamba na kulinda roho za wananchi na heshima yao, atakayekufa katika vita hiyo ni shahidi..

Baada ya wito huo wazee kwa vijana walijitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya vita, walijitolea kupigana wakiwa na hamasa kubwa ambayo ni marachache kushuhudiwa duniani.

Walipigana vita kali kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita, walionyesha ushujaa na ubinaadamu kwa kuwalinda wananchi hadi familia za maadui na kuwapa huduma nzuri za kibinaadamu, katika vita hiyo walikufa kishahidi makumi kwa maelfu na wengine wengi walijeruhiwa, yote hayo ilikuwa ni kwa ajili ya kuokoa taifa na maeneo matakatifu.

Hadi Mwenyezi Mungu mtukufu alipo wapa ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, na wakakomboa maeneo yaliyokuwa yametekwa na magaidi hao na kutokomeza utawala wao, wakawa wameikomboa Iraq na nchi za kieneo pamoja na dunia yote kwa ujumla.

Ushindi ulipatikana kwa sababu mbili kubwa, nazo ni fatwa takatifu na namna wananchi wa Iraq walivyo itikia fatwa hiyo, ardhi ikatetemeka chini ya nyayo za madhalimu waliokuwa wanalitakia shari taifa hili, kwa kusaidiwa na nchi maarufu, tuliwatisha madhalimu pamoja na matarajio makubwa waliyo kuwa nayo.

Kumbuka kuwa kwa mara ya kwanza fatwa hiyo ilisomwa ndani ya haram ya Abul-Ahraar Imamu Hussein (a.s), juu ya mimbari ya swala ya Ijumaa kupitia muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, katika nukta ya nne alisema kuwa:

(Hakika kuwasaidia watoto wetu na askari wote ni jambo tukufu, inakuwa lazima kufanya hivyo pale inapo bainika kuwa magaidi wana mwenendo wa dhulma uko mbali na mafundisho matukufu ya Uislamu, hawataki kuishi na watu kwa amani, wanafanya ukatili na kumwaga damu pamoja na kuchochea ubaguzi, hizo ndio nyenzo zao za kupanua utawala kwenye miji tofauti hapa Iraq na kwenye nchi zingine, enyi vijana wetu askari mnajukumu la kizalendo na kisheria, nia yenu na makusudio yenu iwe ni kulinda heshima ya Iraq na umoja wake, pamoja na kuwalinda wananchi na maeneo matakatifu kwa kuwaondoa magaidi hao kwenye nchi hii iliyo dhulumiwa yenye raia waliojeruhiwa.

Pamoja na wito wa Marjaa Dini mkuu wa kuwasaidia na kusimama pamoja na nyie, mnatakiwa muwe mashujaa wenye msimamo na subira, atakaye uwawa katika vita hii atakuwa amekufa shahidi, wazazi wanatakiwa kuwahimiza watoto wao na mke amuhimize mumewe aende kupigana kwa ajili ya kulinda taifa hili na raia wake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: