Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimemaliza hatua ya maandalizi ya ujenzi wa kituo cha Ahayaat katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna.

Tumeongea na Swafaa Muhammad Ali mmoja wa wasimamizi wa mradi huo amesema kuwa: “Baada ya kumaliza kuandaa mchoro wa mradi na kukubaliana na upande wa wanufaika, jana tumekamilisha kazi ya kusawazisha kiwanja na kumwaga zege kwa (BRC)”.

Akaongeza kuwa: “Sasahivi tunaendelea na vipengele vingine baada ya kuchukua vipimo vya ardhi pamoja na kuiandaa kwa ajili ya msingi”.

Akabainisha kuwa: “Kuna kazi nyingine inaendelea vizuri pia, nayo ni kujenga umbo la boma kwa kutumia vyuma na kuhakikisha kazi inakamilika ndani ya muda tuliokubaliana”.

Kumbuka kuwa mradi huu upo chini ya ufadhili wa idara ya afya ya mkoa wa Muthanna chini ya hospitali ya Husseini (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: