Kuendeleza vipaji vya vijana na kuwarekebisha kifikra ni miongoni mwa malengo makubwa ya jumuiya ya Skaut ya Alkafeel

Maoni katika picha
Idara ya harakati na mahema katika jumuiya ya Skaut ya Alkafeel, chini ya ofisi ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari, inaendeleza vipaji vya watoto na vijana kwenye sekta zote.

Kiongozi wa idara ya watoto na makuzi Ustadh Hasanaini Faruuq ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inamalengo mengi, ambayo imekuwa ikiyafanyia kazi ndani ya kipindi cha miaka mitano, kupitia ratiba zake na mafundisho mbalimbali yanayo kidhi mahitaji ya mtu na jamii, mafunzo yenye malezi mazuri kwa washiriki yanawajenga kidini na kibinadamu, yanawaongezea maarifa na elimu pamoja na kujitambua”.

Akaendelea kusema: “Hakika mafunzo yetu yanakomaza akili ya mtu na kukuza vipaji vya washiriki, na yanawawezesha kujilinda dhidi ya fikra potofu, sambamba na kuwajengea uzalendo na mapenzi ya taifa lao pamoja na dini yao”.

Akasema: “Mafundisho mbalimbali ya Skaut, michezo, mazowezi, safari yote yanafanyika katika Skaut”.

Akafafanua kuwa: “Malengo ya Skaut yanaonekana wazi kupitia mafundisho tofauti yanayo tolewa na jumuiya hiyo ndani ya kipindi chote cha mwaka, mafunzo ambayo wanashiriki maelfu ya vijana wenye umri wa miaka (7) hadi (17), sambamba na kutumia muda wa likizo za shule vizuri na kunufaika nao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: