Watumishi wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji wanaendesha opresheni ya kupuliza dawa katika chuo kikuu cha Alqadasiyya

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wanapuliza dawa katika chuo kikuu cha Alqadisiyya/ Mkoani Diwaniyya.

Opresheni hiyo inatokana na ombi la chuo hicho kwa kikosi, ndipo wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) katika mkoa wa Diwaniyya wakaamua kufanya kazi ya kupuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Msemaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) ameripoti kuwa: Kazi ya kupuliza dawa imefanywa baada ya kupokea maombi kutoka vitivo tofauti vya chuo kwa lengo la kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Uongozi wa chuo umeshirikiana na watumishi wa kikosi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tambua kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona mara tu baada ya kugundulika virusi hivyo, kimekuwa kikipuliza dawa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye nyumba za makazi ya watu, ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: