Kituo cha matangazo na masoko Alkafeel kimempokea mkuu wa mkoa wa Karbala kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano

Maoni katika picha
Kituo cha matangazo na masoko Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya leo siku ya Jumapili (21 Shawwal 1441h) sawa na (14 Juni 2020m) kimempokea mkuu wa mkoa wa Karbala Sayyid Naswifu Khatwabi, na kujadili namna ya kushirikiana kati ya kituo na mkoa, na wamekubaliana kuongeza ushirikiano kwa faida ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Mkuu wa mkoa amepokelewa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Maitham Zaidi na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Sayyid Mustwafa Dhiyau-Diin pamoja na mkuu wa kituo hicho Ustadh Muhammad Aali Taajir, ambae amesema: “Kuna mambo muhimu yatafanywa na kituo hiki siku za mbele, yatakayo saidia katika ujenzi wa mkoa, sambamba na kulinda utambulisho wa Dini na malikale”.

Kumbuka kuwa kituo cha matangazo na masoko Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Ataba tukufu, siku za nyuma kilimpokea waziri wa vijana na michezo Sayyid Adnani Darjali na ujumbe alio fuatana nao, wakajadili namna ya kuboresha ushirikiano baina yao, walikuwa wamesha kubaliana kuimarisha ushirikiano baina yao na viongozi walio tangulia, kwenye sekta ya habari za namba au kwenye mitandao, pamoja na kuweka namba kama alama ya kudumu, yote hayo yatafanywa chini ya kanuni na taratibu za kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: