Kumaliza ukarabali wa barabara ya Alqami

Maoni katika picha
Katika kuendelea na ukarabati wa barabara zinazo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi ya kuweka lami barabara ya Alqami imekamilika, nayo ni barabara muhimu, kazi hiyo imefanywa na uongozi wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu pamoja na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu Sayyid Naafi Mussawi, amesema: “Barabara ya Alqami ilikuwa imeharibika sana, kwani inamuda mrefu bila kufanyiwa ujenzi, ubovu wa barabara hiyo ulikuwa unatatiza utembeaji wa mazuwaru wanao kwenda katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuharibu vyombo vya usafiri pia, ndipo watumishi wa kitengo cha usimamizi wa eneo la katikati ya haram mbili takatifu na kitengo cha usimamizi wa kihandisi wakaamua kuifanyia matengenezo na kuiweka lami kuanzia mwanzo wa barabara hadi kwenye kituo cha Hauraa na barabara inayo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), matengenezo yote yamefanywa kwa kuzingatia muonekano asili wa barabara bila kuweka mabadiliko yeyote”.

Mhandisi Alaa Hamza Salmani kiongozi wa idara ya ufundi katika kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu amesema kuwa: “Eneo lililotiwa lami katika barabara hiyo linaurefu wa mita za mraba (200) na upana wa mita (5) pamoja na vipande vya barabara ndogo zinazo katisha kwenye barabara hiyo hadi kwenye kituo cha Hauraa kuelekea mlango wa Bagdad kwa upande wa kulia, na kwa upande wa kushote inaelekea kwenye mlango wa Kibla, watumishi wa vitengo viwili tulivyo tajwa wamefanya kazi zote za awali, ikiwa ni pamoja na kusawazisha mashimo, kuondoa nyaya za umeme ambazo zingetatiza upitaji wa gari za kutengeneza barabara na kuweka lami, pamoja na kuondoa vituo vya ukaguzi vilivyo kuwepo mwishoni mwa barabara, na kuondoa kila kitu ambacho kingetatiza shughuli hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: