Mtazamo wa kituo cha kiislamu katika masomo ya kimkakati ya elimu za kimagharibi

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa mtazamo kuhusu elimu za kimagharibi, kupitia chapisho la jarida la kwanza liitwalo (majadiliano kuhusu elimu za kimagharibi) yaliyo fanywa na watafiti wa kimataifa wa kiarabu na kiislamu, jarida hilo limeandaliwa na kuandikwa na jopo la wabobezi katika kituo tajwa, aidha ni sehemu ya muendelezo wa machapisho yao, (mradi wa taasisi za elimu za kimagharibi) ambazo zimeonyesha uzowefu wa kimagharibi kupitia mitazamo ya waarabu na waislamu wanao safari.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Sayyid Hashim Milani kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel, amesema kuwa: “Kitabu hiki cha majadiliano kinaingia katika mfumo wa mkakati wa kimaarifa uliopangwa na kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati, katika kubainisha mtazamo wa elimu za kimagharibi, tunawaletea wasomaji mfululizo wa majadiliano ya watafiti wa mambo ya falsafa, siasa na jamii katika ulimwengu wa kiarabu na kiislamu”.

Akaongeza kuwa: “Maswali yaliyo ulizwa yalikuwa yanalenga kuwafahamu wamagharibi, kila mshiriki ametoa maoni yake kuhusu utamaduni wa kiarabu na kiislamu pamoja na ule wa kimagharibi, kuanzia harakati za ulaya na zama za ukoloni hadi miongo ya zama zetu”.

Mwisho Sayyid Milani akatoa shukrani kwa kila mtu aliyechangia kufanikiwa kwa uandishi wa kitabu hiki, kuanzia watafiti, wahariri na wafasiri, ambao wamefanya kazi kubwa ya kuwezesha kuchapishwa hiki kitabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: