Matibabu ya kisasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel bila kufanya upasuaji

Maoni katika picha
Kituo cha tiba katika hospitali ya rufaa Alkafeel kinamiliki kifaa cha kisasa kinacho weza kutibu mtu mwenye tatizo la kufanyiwa upasuaji bila kumpasua.

Daktari bingwa wa upasuaji bwana Muhammad Sami amesema kuwa: “Tangu kufunguliwa kwa kituo hiki tumesha pokea wagonjwa wengi ambao wangetakiwa kufanyiwa upasuaji lakini tumewatibu bila kufanya upasuaji”.

Akabainisha kuwa: “Magonjwa tunayotibu ni tatizo la mgongo na shingo, pamoja na matatizo ya viungo kama vile mikono, magoji, miguu pamoja na maradhi mengine tofauti”.

Akafafanua kuwa: “Maradhi hayo hutibiwa kwa njia ya upasuaji lakini kwa kutumia teknolojia ya kisasa mgonjwa anaweza kutibiwa bila kupasuliwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: