Idara ya kuhifadhisha Quráni inandelea na masomo kwa njia ya mtandao ikiwa na washiriki (80) ambao ni mahafidh

Maoni katika picha
Idara ya kuhifadhisha Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendesha semina kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi (80) walio hifadhi Quráni, mitandao ya mawasiliano ya kijamii inawawezesha kujisomea maranyingi na kuhifadhi.

Semina hii kwa njia ya masafa inafanyika kutokana na maelekezo ya wizara ya afya ambayo imepiga marufuku misongamano ya watu, aidha tunatekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu aliye kataza misongamano ya watu kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Hii ni moja ya semina nyingi zitakazo fanywa kwa njia ya mtandao na Maahadi pamoja na matawi yake yaliyopo mikoani kwa lengo la kuongeza uwezo wa usomaji wa Quráni na kuihifadhi, huku wanafunzi wakiendelea na masomo wakiwa salama majumbani kwao, kuendeleza miradi ya Quráni ni kuvitumikia vizito viwili vitakatifu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kila mwaka hufanya harakati za Quráni, lakini kutokana na mazingira ya sasa ambayo taifa linapitia pamoja na hatua ambazo Atabatu Abbasiyya imechukua kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, mwaka huu tutatosheka na harakati chache zitakazo fanywa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: