Bwana Swafaa Muhammad Ali Mhandisi mtendaji wa mradi huo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa, mafundi wanatarajia kukamilisha mradi huu ndani ya muda ulio kusudiwa na kwa ubora unaotakiwa”.
Akasema kuwa: “Kazi zimefika katika hatua zifuatazo:
- - Umekamilika ujenzi wa boma la juma katika hatua ya kwanza na tumeingia hatua ya pili.
- - Tumeanza kazi ya kukata vyumba kwa kutumia (Sandweeg panel).
- - Tumeanza kazi ya kumwaga zege ya hatua ya tatu na ya mwisho kwenye eneo la uwanja wa kituo.
- - Tunaendelea na kazi ya kuweka bomba za maji taka pamoja na bomba makuu za usambazaji wa maji safi”.
Akaongeza kuwa: “Kazi zote zinaendelea kama zilivyo pangwa bila kuwepo na muingiliano wowote, aidha kazi ya kufunga nyaya za umeme pia imeanza, na ufungaji wa (jipsambord) utaanza hivi karibuni”.
Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo hiki unaofanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya unatokana na mchango wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kuongeza uwezo wa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, kituo hicho kinaukubwa wa mita za mraba (3500) kitakuwa na vyumba (114) vyenye kila kitu cha lazima katika vifaa tiba.