Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Samiri Abbasi amesema kuwa, changamoto kubwa wanayo pata mafundi wanaojenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Bagdad, Karbala na Muthanna, ni ukaribu wake na vituo vya afya.
Akaongeza kuwa: “Pamoja na mazingira kuwa magumu lakini sio sababu ya kuchelewesha ujenzi, mafundi wetu wana afya nzuri na wanafanya kazi kwa kufuata kanuni zote za kujilinda na maambukizi ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa”.
Akaendelea kusema: “Mafundi wetu walifanikiwa kujenga vituo vitatu vya kwanza bila kusajili tukio lolote la maambukizi baina yao, kutokana na tahadhari wanazo chukua, aidha wanamaliza kazi haraka ndani ya muda ulio pangwa, nimatumaini yetu kuwa watakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha nne, cha tano na cha sita ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa”.