Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa kike kwenye mimbari za Husseiniyya inaanza msimu wa masomo kwa njia ya mtandao.

Maoni katika picha
Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya wahadhiri wa kike kwenye mimbari za Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza msiku wa pili wa mwaka wa masomo kwa njia ya mtandao, inatumia mawasiliano ya mitandao ya kijamii kuwasilisha masomo kwa wanafunzi wa hatua zote.

Makamo kiongozi wa wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Maahadi hiyo Ustadhat Taghridi Abdulkhaaliq Tamimi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Matumizi ya njia ya mtandao yamesababishwa na tatizo la maambukizi ya virusi vya Korona na maagizo ya wizara ya afya pamoja na kutopoteza mwaka wa masomo kwa wanafunzi”.

Akaongeza kusema: “Tumeandaa ratiba kamili ya masomo kwa wanafunzi wa ngazi zote, pamoja na kozi ya Batuli na Nuru-Zaharaa zitakazo tolewa sambamba na msimu huu wa masomo, tayali wanafunzi wameambia muda wa masomo kama ifuatavyo:

  1. Ngazi ya Tamhidi, hatua ya kwanza, ya pili na ya tatu: siku za masomo ni Jumapili hadi Jumatano.
  2. Kozi ya Batuli na Nuru-Zaharaa siku ya Ijumaa na Jumamosi.
  3. Kozi ya mihadhara kwa lugha ya kiengereza siku ya Ijumaa na Jumamosi”.

Akasema: “Wakufunzi wa Maahadi wamejiandaa kufundisha kwa kila aina ya njia, aidha wanafunzi nao wapo tayali kuanza masomo”.

Kumbuka kuwa lengo la kuanzishwa kwa Maahadi hii ni kuwajenga wanawake kitablighi hususan wakati wa miezi ya kuomboleza na kuwatoa pembezoni katika kuhadithia tukio la Imamu Hussein kwa kutumia njia na mfumo unao eleweka na unaokaribiana na uhalisia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: