Kituo cha turathi za Karbala ni sehemu inayo fichua yaliyo sahauliwa na historia katika mji huu

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala ni moja ya vituo vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, vilivyopo kwenye mikoa tofauti ya Iraq vyenye jukumu la kufichua malikale za taifa hili na kuandika vitabu vinavyo elezea malikale hizo.

Mkuu wa kituo tajwa Dokta Ihsani Gharifi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kituo cha turathi za Karbala kinajukumu la kukusanya na kufanya utafiti kuhusu malikale zote za mji mtukufu wa Karbala, kuanzia vifaa, picha, athari za kielimu, wanachuoni na viongozi pamoja na kuchapisha majarida na kuendesha semina zinazo husu mali kale, kwa lengo la kukifanya kituo hiki kuwa sehemu ya kurejewa na watafiti wote”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kinalenga kuhifadhi turathi za Karbala na kuzifanya kuwa kimbilio la waandishi wa historia kwa manufaa ya wanafunzi na wadau wa elimu, aidha kuwa sehemu ya utambuzi wa fani tofauti na viongozi wa Karbala pamoja na kuenzi utukufu wao, na kuonyesha ukongwe wa mji kwani Karbala ni miongoni mwa miji ya Kihistoria”.

Akasema: “Umuhimu wa kituo cha turathi za Karbala ni kuwa kitovu cha harakati za kijamii na kitamaduni, kinatunza utambulisho wa jamii na utamaduni wa vizazi na vizazi, mazingira ya mji wa Karbala yanaonyesha undani wa historia, mji huo ulikuwa kinara wa harakati za kidini, kijamii, kisiasa, kiuchumi na vingine vingi vilivyo kuwepo katika jamii ya waislamu”.

Kumbuka kuwa kituo kipo katika mkoa wa Karbala/ mtaa wa Baladiyya, anuani ya barua pepe ni: turath@alkafeel.net au kupitia toghuti yake: http://www.mk.iq/cen.php?id=1 au simu ya mezani: (310058) na simu ganja: (07810528170).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: