Madaktari wa kiiraq na kigeni wamefanya maelfu ya upasuaji katika Hospitali ya Alkafeel

Maoni katika picha
Hospitali ya Alkafeel iliyopo Karbala inamadaktari wa kiarabu na kigeni wenye umahiri mkubwa na ubobezi wa mambo tofauti.

Kiongozi wa kitengo cha upasuaji Dokta Osama Abdulhassan amesema kuwa: “Miaka ya nyuma hospitali ilitowa mchango mkubwa wa majeruhi wa Hashdu Shaábi, na kuwafanyia upasuaji ambao ungewalazimu kwenda nje ya taifa”.

Akabainisha kuwa: “Jopo la madaktari wa kiiraq na kigeni limefanya maelfu ya upasuaji, na asilimia kubwa ya upasuaji wao ulifanikiwa, haspitali hualika madaktari wa kigeni wenye ujuzi na uzowefu mkubwa katika kutibu magonjwa mbalimbali”.

Akafafanua kuwa: “Hospitali ilifanya upasuaji wa aina tofauti ukiwemo upasuaji wa moyo kwa watoto wadogo, upandikizaji wa figo, uwekaji wa viungo bandia na matibabu ya ubongo chini ya madaktari bingwa wa kimataifa”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel wakati wote inatoa huduma bora kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa inavyo miliki pamoja na umahiri wa madaktari bingwa ilionao kutoka ndani na nje ya nchi.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa waliopo katika hali zote za maradhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: