Tambua kazi za idara ya upambaji katika matukio ya kidini

Maoni katika picha
Kazi kubwa inafanywa na watumishi wa idara ya mapambo chini ya kitengo cha uangalizi wa haram takatifu ya Atabatu Abbasiyya katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuhudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), hususan katika matukio tofauti ya kidini, kumbukumbu za vifo au kuzaliwa.

Kiongozi wa idara tajwa Ustadh Hassanaini Swadiq Kadhim Alquraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi nyingi zinafanywa na idara yetu, miongoni mwa kazi hizo ni kuweka mapambo ya vitambaa vyeusi na mabango yaliyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni katika matukio ya misiba, kama vile Ashura, Arubaini na matukio mengine ya misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na kuweka mapambo mazuri wakati wa matukio ya kukumbuka kuzaliwa kwa Maimamu watakatifu (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Idara ya ushonaji katika kitengo cha zawadi na nadhiri huchukua vipimo vya sehemu zinazo kusudiwa kupambwa, halafu hushona mapambo yanayo endana na maeneo hayo kwa umakini mkubwa”.

Akasema kuwa: “Kazi hufanywa kwa kutumia vifaa maalum ikiwa ni pamoja na winchi kwa ajili ya kufikia sehemu za juu katika Ataba tukufu, na mapambo huwekwa kwa umaridadi mkubwa”.

Tambua kuwa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu kina majukumu mengi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kufagia, kupiga deki, kutandika miswala na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: