Tambua hatua za ukarabati katika makumbusho ya malikale na makhtutwaat Alkafeel

Maoni katika picha
Hazina ya makumbusho ya malikale na makhtutwaat ya Alkafeel inavifaa vingi vya kale, miongoni mwa vifaa hivyo ni vile vilivyokuwa vikitumiwa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya wa zamani ndani ya haram ya malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa maelezo zaidi kuhusu ukarabati wa malikale katika kitengo cha makumbusho, tumeongea na kiongozi wa idara hiyo Ustadh Hussein Ali Ma’maar amesema kuwa: “Makumbusho inavifaa vingi vya zamani vyenye uharibifu tofauti kutokana na kukaa muda mrefu, ukarabati wa vifaa hivyo hupitia hatua zifuatazo:

Kwanza: kupiga picha kifaa husika.

Pili: kama kifaa kimenakshiwa kwa madini (nakshi za fedha) huanza kutolewa madini hayo kisha kukarabati kifaa husika halafu ndio kinarudishiwa nakshi zake za madini zilizo kuwepo.

Tatu: sehemu ya madini (nakshi za madini) na katika kuondoa mipasuko hutumiwa (meganol) na vifaa vya plastiki pamoja na kusafisha sehemu hiyo kwa kutumia kemikali pamoja na pamba.

Nne: hurudishiwa vipande vilivyo tengenezwa na kuvigundisha pamoja kwa kutumia (B72) asilimia %2 na baada ya siku (15) huwekwa kwa mara ya pili kwa asilimia %5 kwa ajili ya kulinda athari za nje.

Kumbuka kuwa makumbusho ya malikale na makhtutwaat ya Alkafeel ni miongoni mwa makumbusho za kwanza kufunguliwa na Ataba za Iraq, ilifunguliwa mwaka (2009) katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), makumbusho hiyo inavifaa vingi vya zamani vyenye mamia ya miaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: