Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi kwa kushirikiana na taasisi ya Dhabiih wameshona barakoa (6000) na kuzigawa bure

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Sha’abi) katika mkoa wa Basra kupitia watumishi wake kwenye wilaya ya Zuberi, wamefanikiwa kushona barakoa (6000) kwa kushirikiana na taasisi ya Dhabiih, na wamezigawa bure kwa vikundi mbalimbali na taasisi za serikali na za kiraia, chini ya mkakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa walianza kushona barakoa tangu lilipo ripotiwa janga la virusi vya Korona, na wameendelea kushirikiana na taasisi ya Dhabiih idara ya wanawake katika ushonaji wa barakoa, bidhaa ambayo inahitajika sana kwa sasa, tumeongeza uzalishaji wa barakoa kwa kufungua kituo kingine cha wanawake katika ofisi za makao makuu.

Akabainisha kuwa: barakoa zilizo shonywa tumezigawa katika vituo vya afya vya Basra –wilaya ya Zuberi- na kwenye hospitali ya Fihaai na hospitali ya maradhi ya saratani ya mkoa wa Basra.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kimekuwa kikipuliza dawa sehemu za makazi ya watu, ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pamoja na kushona barakoa na kuzigawa kwa wananchi, aidha kimekuwa kikitoa misaada ya kibinaadamu kwa wahanga na kinafanya kila kiwezalo katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: