Kitengo cha usimamizi wa kihandisi: kukamilika silimia %70 ya ujenzi wa boma la chuma katika kituo cha Alhayaat cha sita mkoani Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha asilimia %70 ya ujenzi wa boma la chuma katika mradi wa kituo cha sita cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Muthanna.

Mhandisi mtendaji wa mradi bwana Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ujenzi wa boma la chuma umepiga hatua kubwa, tayali ujenzi wa hatua ya kwanza na ya pili umekamilika na sasa unaendelea katika hatua ya tatu”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wetu wameanza ujenzi wa nyumba za chini zenye jumla ya vyumba (114) pamoja na kusambaza bomba za maji kazi ambayo imekamilika kwa asilimia %30”.

Akasema kuwa: “Kazi ya kukata (Sandweej panel) bado inaendelea, imekamilika kwa asilimia %40, kazi hiyo inafanywa pamoja na kazi ya kuweka nyaya za umeme”.

Kumbuka kuwa kituo hiki kinajengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500), jengo litakuwa na vyumba (114) vyenye ubora na vigezo vinavyo hitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: