Chini ya timu cha wizara: kituo cha mbinu za ufundishaji kimeandaa warsha kuhusu program zilizo tengenezwa na wairaq (program ya siraji ikitumika kama mfano).

Maoni katika picha
Kituo cha taaluma Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la wataalam wa wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, kimeandaa warsha kuhusu program za ufundishaji kwa njia ya mitandao iliyo tengenezwa na mikono ya wairaq (program ya siraji ikitumika kama mfano).

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Saamir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya wizara kuamua kufanya mitihani ya wanafunzi wa chuo kwa njia ya intanet na kufungua milango kwa vyuo kuchagua program watakazo tumia katika kutoa mitihani, chuo kikuu cha Alkafeel kimechagua (program ya Siraji) ambayo imekuwa ikitumiwa na chuo hicho kwa misimu miwili sasa, ilianza kutumiwa tangu lilipo zinduliwa jengo la pili la chuo cha Alkafeel katika mji wa Najafu tarehe (14 Alprili 2019m)”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya jopo la wataalam wa wizara kuangalia program hiyo walikua na matokeo chanya kutokana na vitu vilivyomo kwenye program hiyo, ukizingatia kuwa imetengenezwa na raia wa Iraq”.

Akaendelea kusema: “Kwahiyo kunaumuhimu wa kufanya warsha kuhusu program za ufundishaji zilizo tengenezwa na wananchi wa Iraq, na ikachaguliwa program ya Siraji kama mfano, wahadhiri wa warsha hiyo ni Dokta Aamir Salim Amiir na Wasam Ali Khuzáli”.

Akabainisha kuwa “Warsha itafanywa siku ya Jumanne (23/06/2020m) kwa kutumia program ya (ZOOM Cloud Meetings) saa tatu jioni na washiriki watapewa vyeti”.

Kwa maelezo zaidi piga namba zifuatazo: (07602323004 / 07711711190).

Kumbuka kuwa kituo cha taaluma Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kiliandaa semina nyingi kwa njia ya intanet (free coll conference) ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa kushirikiana na jopo la wataalam wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: