Katika mwezi mtukufu wa Dhulqaáda tunakumbuka kuzaliwa kwa mkarimu wa watu wa nyumba ya Mtume bibi Fatuma Maasuma (a.s)

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwaka wa (173h) alizaliwa bibi Fatuma Maasuma mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) na dada wa Imamu Ali Ridhwa na shangazi wa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) aliye zikwa katika mji mtukufu wa Qum, naye ni dada mtakatifu aliyetaka kuungana na kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) katika mji wa Khurasani, baada ya kuitwa na khalifa wa bani Abbasi aitwae Ma-amun, akiwa njiani anamfuata kaka yake aliugua na akafariki kisha akazikwa katika mji wa Qum, kaburi lake limekua kitovu cha elimu, Imamu Aljawaad (a.s) anasema: (Atakae mzuru akiwa anatambua haki yake ataingia peponi).

Bibi Fatuma (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina mwanzoni mwa mwezi wa Dhulqaáda mwaka wa (173h) kwa mujibu wa kauli sahihi. Akakulia katika nyumba ya baba yake Imamu Mussa Alkadhim (a.s), akajulikana kwa sifa ya mkarimu wa Ahlulbait (a.s).

Bibi Fatuma (a.s) alikuwa chini ya uangalizi wa kaka yake Imamu Ridhwa (a.s), kwa sababu mwaka alio zaliwa baba yake aliwekwa jela na kiongozi wa bani Abbasi, akawa anahamishwa jela moja hadi nyingine, hadi alipo uwawa kwa sumu mwaka wa (183h).

Imepokewa kuwa kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) alimpa jina la “Maásuma” pia imepokewa kuwa babu yake Imamu Swadiq (a.s) alimpa jina la “Mkarimu wa Ahlulbait” kabla ya kuzaliwa na mama yake, naye ni katika watoto bora zaidi wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) na mwenye daraja kubwa, kaburi lake lipo katika mji wa Qum amejengewa kubba kubwa na eneo pana la haram lenye harakati tofauti, naye ni burudisho la macho ya watu wa Qum na kimbilio lao, watu hufunga safari kila mwaka kwenda kufanya ziara na kutafuta thawabu za kumzuru (a.s).

Bibi Maasuma (a.s) aliishi na ndugu zake chini ya uangalizi wa kaka yake Imamu Ridhwa (a.s) wanahistoria wameandika kuwa watoto wa Imamu Kaadhim (a.s) walikuwa vinara wa uchamungu, imepokewa katika riwaya kuwa Imamu Ridhwa (a.s) alimuambia Saádi Ashaári Qummiy kuwa: (Ewe Saádi mnakaburi letu?) nikasema: Kaburi la Fatuma bun Mussa (a.s), akasema: (Naam.. atakaemzuru huku akiwa anajua haki yake ataingia peponi), riwaya zinazo zungumzia swala hilo ni nyingi.

Imepokewa kutoka kwa Qadhi Nuru-Llahi katika majaalis Mu-uminina kutoka kwa Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu ana haram nayo ni Maka na Mtume ana haram nayo ni Madina, tambueni kuwa na kiongozi wa waumini ana haram nayo ni Kufa, hakika Qum ni Kufa ndogo, pepo inamilango nane, mitatu ipo Qum, imeshikwa na mwanamke katika kizazi changu anaitwa Fatuma binti Mussa, wafuasi wangu wote wataingia peponi kwa uombezi wake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: