Idara za shule za wasichana Alkafeel inafanya ratiba ya kiibada kwa ajili kuomba dua ya kuondoa balaa

Maoni katika picha
Katika kuitikia wito ulio tolewa na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu, kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi baada ya kuongezeka idadi ya maambukizi ya virusi vya Korona, idara ya shule za wasichana Alkafeel imeandaa ratiba ya kiibada ya kusoma dua ya kuondoa balaa.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani amesema kuwa: “Ujumbe wa Sayyid Swafi ulikuwa wazi, hakika tunahaja ya kutumia siraha ya mitume ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu wakati wa matatizo na balaa, tumuombe Alla atuhurumie na kutuondolea balaa hili, idara ya shule za wasichana Alkafeel imeandaa ratiba ya kiibada itakayo tumiwa kwa muda wa siku arubaini, kuanzia mwanzo wa mwezi wa Dhulqaada hami mwezi kumi Dhulhijja”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba inavipengele vifuatavyo: kutoa sadaka hata kitu kidogo kwa nia ya kuondoa balaa hili, kusoma ziara Ashuraa, kusoma dua ya Amani, dua ya Imamu Ridhwa (a.s), dua ya Imamu Aljawaad (a.s), dua ya Imamu Swadiq (a.s) na kumswalia Mtume na watu wa nyumbani kwake mara (100).

Kumbuka kuwa muwakilishi wa Marjaa Dini kuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Alkhamisi ya mwezi (25 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (18 Juni 2020m) alituma ujumbe wa sauti unao wataka wairaq wote wajikurubishe kwa Mola wao baada ya kuongezeka maambukizi ya virusi vya Korona.

Akasisitiza kuwa: “Habari tunazo sikia kila siku hazitii matumaini, jambo ambalo linatutaka tujikurumishe kwa Mwenyezi Mungu hakika yeye ni muweza wa kuondoa majanga, tunahitaji huruma ili kuokoa taifa na wananchi kutokana na maambukizi ya Korona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: