Mkuu wa Maahadi Ustadhat Manaar Jawadi Jiburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya harakati zilizo zoweleka kufanywa na Maahadi, kwa ajili ya kuongeza kiwango cha kushikamana na utamaduni wa Quráni kwa wanawake”.
Akabainisha kuwa: “masharti ya kujiunga na mashindano ni haya yafuatayo:
- - Mashindano haya ni maalum kwa ajili ya wanawake tu.
- - Maudhui za kitabu zihusu Quráni tukufu, sura na aya zake pamoja na matamshi yake.
- - Kitabu kisiwe na mlengo wa kujenga chuki na ugonvi.
- - Kitabu kisiwe kimesha wahi kuandikwa au kutolewa na watu wengine.
- - Kiandikwe kwa hati ya (simplified Arabic) kwenye karatasi ya (A4), kurasa zake ziwekwe namba na kiwe na maneno yasiyopungua (5000) na yasiyozidi (15000)”.
Akaongeza kuwa: “Vitabu vyote vitawasilishwa kwenye kamati ya majaji, mwisho wa kupokea vitabu hivyo ni tarehe (1 Oktoba 2020m).
Kuna zawadi kwa washindi watatu wa kwanza ambazo ni:
Mshindi wa kwanza: 150,000 dinari za Iraq.
Mshindi wa pili: 100,000 dinari za Iraq.
Mshindi wa tatu: 75,000 dinari za Iraq.
Pamoja na zawadi zingine zitakazo gawiwa kwa washindi kumi wa mwanzo”.
Akasema: “Washiriki wapeleke kazi zao moja kwa moja kwenye ofisi za Maahadi ya Quráni tukufu kitengo cha wanawake mjini Najafu/ mtaa wa Hanana, au kwenye matawi yake yaliyopo mikoani, aidha wanaweza kutuma kwa barua pepe ifuatayo nafhat296@gmail.com”.