Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Bagdad: wanafunzi 288 wanasoma kwa njia ya mtandao katika maeneo mengi ya mji mkuu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inaendelea kufundisha kwa njia ya mtandao, wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tawi la Bagdad wanaendele na masomo kwa App tofauti, chini ya walimu wabobezi ambao wanahakikisha usalama kwa wote na kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tawi limetoa zaidi ya semina (30) katika maeneo yote ya mkoa na jumla ya wanafunzi (288) wameshiriki kwenye semina hizo, semina zimehusu (masomo ya kitafiti, hukumu za usomaji wa Quráni, visomo kumi, kuhifadhi Quráni na vikao vya usomaji wa Quráni), tumechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Masomo hayo ni sehemu ya kukamilisha ratiba iliyokua imesimama kwa sababu ya hatari za kiafya, wataendelea kufundisha kwa njia ya masafa ili kukamilisha mtaala wa masomo.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kila mwaka hufundisha mambo mbalimbali kuhusu Quráni, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa na hatua zilizo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, mwaka huu tutatoshoka na mambo machache.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: