Maeflu ya vitabu vimewekwa kwenye mtandao na maktba ya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya watafiti

Maoni katika picha
Miongoni mwa vitu vya msingi vinavyo fanywa na kituo cha taaluma za namba chini ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya, ni kurahisisha upatikanaji wa vitabu vinavyo saidia katika utafiti pamoja na uandishi wa vitabu.

Maktaba inamaelfu ya vitabu vya fani tofauti vilivyo andikwa kwa kiarabu na kiengereza, kituo hupokea maelfu ya faili kwa njia ya mtandao kutoka sehemu tofauti, huziandaa na kuziingiza katika mfumo wa taaluma ya namba, halafu huwekwa wazi kwa watafiti na wanufaika kwa njia rahisi.

Ustadh Ammaar Hussein Jawaad mkuu wa kituo cha taaluma za namba ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Tunapokea taarifa nyingi na kuziingiza katika mfumo wa taaluma za namba, zinahusisha vitabu na nyaraka za kitafiti zenye ripoti tofauti, pamoja na zisizokuwa na faida yeyote, huwa tunafanya uchambuzi na kuondoa nyaraka zinazo jirudia rudia pamoja na zisizofaa, halafu hubakiza zilizo bora na zenye manufaa tu”.

Naye Ustadh Aisar Shimmir mkuu wa kitengo cha matamko katika kituo amesema kuwa: “Jumla ya nyaraka zilizo tufikia hadi sasa ni zaidi ya milioni kumi (sio vitabu), tumechambua na kupata chini ya mada laki moja zinazo faa lakini kazi bado inaendelea, na tumeandika zaidi ya anuani elfu sitini”.

Kumbuka kuwa kituo cha taaluma za namba kinamchango mkubwa wa vitabu vya kwenye mtandao, hukusanya mazujuu tofauti ya muandishi mmoja na kuyaweka kwenye faili moja, kwa mfano juzuu kumi (10) huziweka kwenye faili ya (PDF) na kuwa sawa na kitabu kimoja, hivyo kituo hiki ni miongoni mwa vituo vichache ambavyo vinamrahisishia mtafiti upatikanaji wa vitabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: