Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wanapuliza dawa katika mkoa wa Waasit

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wanapuliza dawa katika mkoa wa Waasit kwa kushirikiana na idara ya mkoa huo na jeshi la wananchi.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: kazi hiyo imefanywa mbele ya kamanda wa ulinzi wa mkoa wa Waasit Haani Muhsin Dakhil, sehemu zilizo pulizwa dawa ni Samiir Maksuus (CBRN) na kwenye nyumba za makazi ya watu, barabara, soko na maeneo mengine, jumla ya lita (10,000) za dawa zimetumika.

Akafafanua kuwa baada ya kuongezeka idadi ya maambukizi, na kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa mkoa huo ndipo kikosi cha Abbasi kupitia wawakilishi wake kikaamua kufanya shughuli hii.

Tumelenga maeneo yaliyokuwa na maambukizi pamoja na sehemu zingine.

Akasema kuwa tumepuliza dawa sehemu zote ambazo watu hukusanyika kwa kushirikiana na idara ya afya pamoja na jeshi la wananchi na wadau wengine.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi kiliunda kamati maalum ya kupambana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona, na imekuwa ikipuliza dawa sehemu mbalimbali za makazi ya watu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na inafanya kila iwezalo kupambana na janga hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: