Kiongozi wa idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Farasi Abbasi Hamza, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Wito huu umetokana na msongamano uliopo kwenye mfumo huo, unaopokea maelfu ya simu kila siku kwa sababu ya mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, na kufuatia malalamiko ya wahudumu wa afya wanaopambana na janga la virusi vya Korona, tunawaomba waumini wawape nafasi kuanzia saa mbili hadi saa mbili na nusu jioni kila siku”.
Tambua kuwa mfumo huu umeandaliwa na idara ya mawasiliano ya Ataba tukufu kwa kushirikiana na kamati ya habari na mawasiliano, nao unavituo vinne vimegawanywa kila upande wa nguzo ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, kila kituo kina vifaa vinne hadi vitano vya kupokelea simu, ziara hufanywa kwa njia ifuatayo:
- - Mtu anayetumia mtandao wa (Zain, Aasiya na koku) anapiga simu ya bure kwa namba (443).
- - Mtumiaji wa mtandao wa Alkafeel anaweza kupiga moja kwa moja simu ya bure kwa kutumia namba (07602111000).
- - Mtu aliye nje ya Iraq anaweza kupiga simu namba (009647602111000) lakini hiyo sio simu ya bure kwa sababu inaingia katika mfumo wa kimataifa.
- - Baada ya kupiga simu itapokelewa na utaambiwa kuwa upo chini ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) omba shida zako zitajibiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, utahisi upo ndani ya haram tukufu na utafanya ziara.
- - Muda wa ziara utakaopewa ni dakika moja, simu itakatika moja kwa moja baada ya muda huo.
- - Wakati wa kupiga simu utaona upo katika mazingira ya ziara na unatakiwa usome ziara kwa ufupi.
- - Mfumo huo unapokea zaidi ya simu (1000) kwa saa bila tatizo lolote.
- - Simu zote ni bure ispokuwa zinazo toka nje ya nchi.