Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimesema kuwa: mradi wa ujenzi wa boma la chuma na kukata (Sandwich panel) katika kituo cha Alhayaat cha sita kwenye mkoa wa Muthanna umekamilika kwa asilimia %85

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamekamilisha asilimia %85 ya ujenzi wa boma la chuma katika mradi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Muthanna, kazi ya kukata (Sandwich panel) imekamilika kwa asilimia %85 pia.

Mhandisi mtendaji wa mradi Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Sehemu iliyobakia katika ujenzi wa boma la chuma, ni ile iliyo bakizwa kwa ajili ya vyumba vya madaktari na dawa”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea katika hatua zingine sambamba na kufunga nyaya za umeme na kuweka njia za maji”.

Akasisitiza kuwa: “Tunafanya kazi saa (12) kwa siku ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa”.

Kumbuka kuwa kituo hiki kinajengwa kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kuongeza uwezo wa kupokea wagonjwa katika hospitali ya Hussein (a.s) kwenye mkoa wa Muthanna, kituo kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500) kitakuwa na vyumba (114).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: