Kila siku ndani ya wiki nzima: idara ya kujikinga na maambukizi inapuliza dawa kwenye maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya kujikinga na maambukizi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na kazi ya kupuliza dawa kwenye barabara zote zinazo elekea Atabatu Abbasiyya tukufu, jukumu hilo wamepewa baada ya kutokea janga la virusi vya Korona, wamekuwa wakipuliza dawa kila siku bila kupumzika.

Mhandisi Haamid Alawi Hussein kiongozi wa idara ya kujikinga na maambukizi amesema kuwa: “Watumishi wa idara yetu hawaja acha kupuliza dawa katika maeneo yanayo zunguka Ataba na uwanja wa katikati ya haram mbili hata siku moja baada ya kutokea janga la Korona, sambamba na kupuliza dawa kwenye majengo yote yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa: “Kazi yetu inaongezeka kila siku, watumishi wetu wanapuliza dawa sehemu zote zinazo zunguka Ataba tukufu tena kwa umakini mkubwa, na wanazingatia kiwango cha dawa inayo tumika, wanatumia vifaa vyenye ubora mkubwa vilivyo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud”.

Kumuka kuwa idara ya kupambana na maambukizi ni miongoni mwa idara muhimu katika kitengo cha utumishi ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: