Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu linaendelea na ratiba ya vikao vya usomaji wa Quráni kwa kutumia intanet chini ya walimu wabobezi.
Katika mazingira ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona vikao vya usomaji wa Quráni vinaendelea kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii (video call), kwa sababu washiriki wanatakiwa kusoma kwa matamsi sahihi.
Tawi la Maahadi ya Quráni linaendelea na ratiba yake kwa kufundisha masomo tofauti kuhusu Quráni, kutokana na umuhimu wa kufundisha utamaduni wa kufuata mafundisho ya vizito viwili vitakatifu.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imezowea kufundisha masomo mbalimbali kuhusu Quráni, lakini kutokana na hali ambayo taifa linapitia kwa sasa pamoja na tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo chukuliwa na Ataba tukufu, mwaka huu tumetosheka na harakati chache, ikiwemo harakati hii.