Atakaepata maambukizi ya virusi vya Korona kwa sababu ya kutochukua hatua za kujikinga hana udhuru wa kisheria

Maoni katika picha
Katika mwezi wa tatu mwaka huu Marjaa Dini mkuu alisema kuwa inapasa kujikinga na mtu anaye hofiwa kuwa na virusi vya Korona, iwapo hautajikinga halafu ukaambukizwa hautakua na udhuru kisheria.

Aliyasema hayo wakati maambukizi ya virusi vya Korona yalipo anza kuenea hapa Iraq, wakati huo idara ya afya ilikua inaripoti makumi ya maambukizi.

Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani ndani ya mwezi wa tatu ilipokea maswali kutoka kwa waumini, yaliyo jibiwa na Mheshimiwa Sayyid mwezi (27 Rajabu 1441h) sawa na tarehe (23 Machi 2020m) swali lililokuwa linahusu kipengele hicho lilikuwa linasema:

Je ni lazima kujitenga na watu –wanaohofiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Korona- kwa kuacha kuwapa mikono, kuwakumbatia, kuwabusu na mambo yanayo fanana na hayo? halafu inafaa kuamiliana nao bila kuchukua tahadhari za kujikinga kama kuvaa barakoa na zinginezo?

Alijibu kuwa:

(Mtu anaye hofia kuambukizwa virusi kwa kugusana na mgonjwa wa Korona, analazimika kujiepusha kugusana naye, ispokua baada ya kuchukua tahadhari za kujikinga –kama kuvaa barakoa na soksi za mikononi pamoja na vitu vingine vitakavyo mpa matumaini ya kuto ambukizwa, iwapo hatachukua hatua yeyote ya kujikinga halafu akaambukizwa hatakuwa na udhuru kisheria).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: