Kazi ya kujenga moja ya sehemu ya barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kazi ya kujenga moja ya sehemu za barabara ya Kibla ya Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), robo ya mwisho ya barabara karibu na malalo takatifu kuelekea kituo cha ukaguzi.

Kiongozi wa kazi za ujenzi katika kitengo hicho anayesimamia kazi hiyo Mhandisi Muhammad Mustafa Twawiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni sehemu ya kazi nyingi zilizo shuhudiwa katika barabara muhimu inayo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na uongozi wa kitengo cha uhandisi, kazi hii imepewa kipaombele zaidi, na imefanywa kisasa”.

Akaongeza kuwa: “Shughuli mbalimbali zimeshuhudiwa kwenye barabara hii, ilikuwa na mabanda yaliyo jengwa bila mpangilio na yalikua yanaharibu muonekano wa barabara, tumeyatoa na kuweka vizuwizi vya zege vinavyo tenganisha barabara na maduka yaliyopo pembezoni mwake pamoja na kuweka paa kwenye mabanda ya kuhifadhi vitu vya mazuwaru wanaoingia kwenye haram ya Aljuud, aidha tumeongeza upana wa barabara upande wa kulia na kushoto”.

Akafafanua kuwa: “Tumejenga upya baadhi ya mabanda ambayo Ataba inayahitaji katika shughuli zake, kama vile mabanda ya kutunzia miswala, kukagua mabeji na mengineyo, yamejengwa kwa utaratibu mzuri ambao hauharibu muonekano wa barabara na wala hayatatizi harakati za mazuwaru, tumejenga uzio wa zege iliyo wekwa nakshi, unao tenganisha maduka na barabara, uzio huo unaurefu wa mita moja na nusu, baada ya hapo tutaanza kujenga kituo cha ukaguzi kitakacho kuwa tofauti na kile kilicho kuwepo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: