Kamati ya madaktari wa kikosi cha Abbasi cha wapiganaji imetoa wito kwa madaktari na wauguzi wajitolee kusaidia wahudumu wa afya

Maoni katika picha
Kamati ya madaktari katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji imetoa wito kwa madaktari na wauguzi walio nje ya huduma warudi haraka kusaidia wahudumu wa afya katika mikoa tofauti, baada ya kuongezeka idadi ya maambukizi katika mikoa mingi ya Iraq.

Kikosi kimeongeza hali ya tahadhari na kimewaelekeza wawakilishi wake pamoja na vikundi vya kibinaadamu vinavyo fungamana nacho visaidie kutoa huduma za matibabu kwa watu wanao ambukizwa virusi vya Korona kwa kuwapa vifaa vya kusaidia kupumua kama inavyo elekezwa na wizara ya afya ya Iraq pamoja na shirika la afya la kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: