Mhandisi mtendaji wa mradi bwana Muhammad Mustafa Twawiil amesema kuwa: “Watumishi wetu wanafanya kazi za kipekee, wanakimbizana na muda na wanataka kumaliza ndani ya muda uliopangwa pamoja na mazingira magumu ya utendaji, baada ya kumaliza hatua ya nne tumeanza kazi za hatua inayo fuata,ambayo sehemu ya kazi zake tayali tumesha zifanya kwenye hatua iliyo isha, miongoni mwa mambo yaliyo fanywa ni:
- - Kuweka marumaru za ukutani katika sehemu inayo tenganisha kati ya ukuta na Jipsam bord, imekamilika kwa asilia %80.
- - Kukamilisha kazi ya kukata vyumba vya vyoo na vyumba vya mitambo ya viyoyozi ambayo imegawanyika sehemu tatu kama ifuatavyo:
Kwanza: Kuweka kiyoyozi maalum katika kila chumba, kazi hiyo imekamilika kwa asilimia %70, vyumba hivyo vitaendelea kutumika hata baada ya kuisha janga la Korona Insha-Allah.
Pili: kufunga vifaa vya kuingiza hewa safi (AIR FRESH), kazi hiyo imekamilika kwa zaidi ya asilimia %70.
Tatu: kufunga vifaa vya kutoa hewa chafu, vifaa hivyo vinasaidia kuuwa bakteria na kuwatoa nje, kazi hiyo imekamilika kwa asilimia %75.
- - Kufunga mfumo wa kutoa onyo, na kuzuwia moto, kazi hiyo imekamilika kwa asilimia %55.
Akabainisha kuwa: “Pamoja na kujikita katika kazi hizo, kuna kazi zingine zinaendelea sambamba na hizo kama vile kujenga sehemu za kufanyia ibada, maabara na zinginezo, tayali boma la chuma limekamilika na sasa tunakata vyumba kwa kutumia (Sandwich panel), kazi hiyo imekamilika kwa asilimia %60, kuna kazi zingine ambazo zimekamilika kwa asilimia %90, kama vile kuweka marumatu kwenye njia zinazo tenganisha sehemu ya kwanza na ya pili na baina ya hospitali na sehemu zingine”.